Ilikuwa siku ya tarehe 6 Decemba 2018 siku iliyofanyika mahafali ya kwanza kabisa shule ya awali ya Hollywood English Medium Primary school. Shule ilianza ikiwa na wanafunzi 27 ambao wote wamefanikiwa kuhitimu mafundisho ya kuhesabu, kusoma na kuandika hivyo ni jambo la kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kufanikisha hilo.
Mwanafunzi mhitimu Noela Luaho.
Uongozi bora chini ya Mkurugenzi wa shule Ndugu I.Kameka Pamoja na Mwalim Mkuu wa shule Ndugu A. Ntengwi ni mafanikio kwa shule yetu.
Kutoka kushoto ni Makamu wa shule Ndugu Budodi, Mwalim mkuu wa shule Ndugu A. Ntengwi, Mgeni rasmi wa sherehe iyo Madam Neema Kameka kutoka NMB Bank-Mlowo Mbozi, Mkurugenzi wa shule Ndugu I.Kameka mwishoni mwalim wa darasa la awali madam Tumaini Ibrahim.
Vilevile safu imara ya waalimu wa kila idara shuleni kwetu imechangia mafanikio kwa shule yetu, pia shukrani za dhati kwa walim wa darasa la awali Madam Tumain Ibrahim, Madam Rehema Sanga na wengine kwa kuwajenga watoto kuwa na uwezo mkubwa wa kusoma kuandika na kuhesabu.
Wahitimu wakijipanga kuingia kwenye ukumbi wa mahafali yao.
Mgeni rasmi wa tafrija hiyo Mama N. Kameka akiwasili eneo la tukio.
Mwalim Mkuu akihutubia wazazi waliofika siku ya tafrija hiyo.
Mkurugenzi wa taasisi ya Hollywood secondary na shule ya msingi Ndugu, I. Kameka akihutubia katika tafrija hiyo.
Mgeni mwalikwa kutoka Marekani ambaye pia ni dada yake na mkurugenzi wa shule akisalimu wazazi na wageni waliofika.
Picha ya pamoja Mgeni rasmi na wahitimu.
Mgeni Rasmi Mama N. Kameka akihutubia hadhara.
Mgeni rasmi mama N. Kameka alihutubia wazaz na wageni wote waliofika siku hiyo kuhusu umuhimu wa kusomesha watoto shule za awali pia aliushukuru uongozi wa shule kwa kuwa na matokeo mazuri kitaaluma hivyo aliomba kuendeleza juhudi za kutoa elim bora kwenye shule yetu. Pia alimshukuru mwalimu wa watoto hao kuwa ni chachu ya mafanikio ya tafrija hiyo aongeze juhudi za ufundishaji.
Aidha alisisitiza mshikamano baina ya wazazi na waalimu ili kupata mafanikio Zaidi kwenye shule yetu. Zaidi Mama N. Kameka aliwaomba wazazi kuwafungulia Account Bank watoto wao ili kuweza kutunza pesa za kuwalipia ada watoto kuliko kuhifadhi nyumban, kwan Bank ya serikali NMB Bank hawana makato yoyote kwa kutunza pesa zao.
Mgeni rasmi alimaliza kwa kushukuru mwenyezi Mungu kwa kuhitimisha tafrija hiyo pia Mkurugenzi wa shule, Mwalimu Mkuu na idara nzima ya waalimu katika shule yetu.
Kama mama pia Mgeni Rasmi alitoa zawadi ya vinywaji kwa watoto kisha alijumuika kunywa nao pamoja.
MAPICHA PICHA
Katikati ni Mkurugenzi wa taasisi ya Hollywood secondary na shule ya msingi Ndugu, I. Kameka kulia kwake ni Mwalim Frank Kaswalula na kushoto ni Mwalimu Benson Mwakasenga.
Mungu Ibariki Hollywood,
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ni mwema karibu shule ya Hollywood kwa mafanikio ya mtoto wako.
Mawasiliano Zaidi Mkurugenzi wa shule 0758-38-08-03.
Na mwandishi wetu ndugu, Benson Mwakasenga.