Search This Blog

Monday, 1 October 2018

MAHAFALI YA KWANZA HOLLYWOOD ENGLISH MEDIUM PRIMARY SCHOOL

Pongezi za dhati kwa mkurugenzi wa Jumuiya ya Hollywood ikijumlisha shule ya msingi na sekondari Mstaafu Ndugu Izyasi A. Kameka, Hollywood primary school ipo katika mji mdogo wa mlowo ambao uko katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.
Ni miaka kumi toka shule ya secondary imefunguliwa na mwaka wa kwanza kwa mahafali ya kwanza shule ya English medium iliyoko mkoani Songwe Tanzania.
Mahafali hiyo ilifana sana furaha kutoka kwa wazaz Waalimu na wanafunzi waagwa.
Mkurugenzi wa shule ya Hollywood English medium Primary School Mstaafu Ndugu Izyasi A. Kameka katika sherehe hiyo pembeni yake ni Mwalimu Mkuu sekondari Hollywood Ndgu Issa Mwakasendo.

  Shule ilianzishwa mwezi January 2012 kisha kupata usajili MB.04/7/006 pamoja na maerekebisho yake mwaka 2018 ya kupewa EM.15887. 


Mwalimu mkuu Shule ya msingi Hollywood Ndugu Abraham Ntengwi akitoa risala siku hiyo.
Akisoma risala Mwalimu mkuu wa shule alisema "Taaluma ya shule mpaka sasa ni nzuri kwani hakuna mwanafunzi yeyote asiye jua kusoma, kuandika na kuhesabu kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba. Pia shule imeshiriki mitihani ya upimaji darasa la nne kitaifa kwa miaka mitatu, kuanzia 2015, 2016 na 2017"





 Mgeni Rasmi siku hiyo Meneja wa uwanja wa Ndege wa Songwe airport  Pius J . Kazeze akihutubia katika sherehe hiyo.


MATOKEO YA SHULE
1. 2015 - Shule ilishika nafasi ya kwanza katika wilaya ya Mbozi na nafasi ya tatu kwa mikoa miwili ya Mbeya na Songwe.
2. 2016 - Shule ilishika nafasi ya kwanza kwa wilaya ya Mbozi na nafasi ya Kwanza kwa mkoa wa Songwe baada ya kutenganishwa na Mbeya.
3. 2017 - Shule ilishika nafasi ya kwanza kiwilaya na kufanya iendelee kushika rekodi yake bila kutetereka.
Katika sherehe hiyo waliagwa wanafunzi ishirini na nne(24) waliohitimu elimu ya msingi katika shle hii kwa mara ya kwanza. Walianza darasa la kwanza mwaka 2012 jumla wakiwa 25 kati yao wavulana 17 na wasichana 8. Kwa bahati mbaya mwanafunzi mmoja alitoroka masomo dakika za mwisho kabisa.
Wote kwa ujumla wana nidhamu safi hali iliyo washangaza hata wasimamizi na walinzi wakati wanafanya mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi, kuanzia mtihani wa kwanza mpaka mtihani wa somo la mwisho hakuna hata mtoto mmoja alliye omba ruhusa ya kutoka nje kujisaidia. Ilikua wakiingia ni kazi tu mpaka mda wa mtihani ukikamilika ndipo wanatoka nje. Ama kwa hakika vijana hawa ni kizazi bora cha shule yetu.



 Waalimu wa wahitimu Mkono wa kushoto Madam Invyolata (Mwalimu wa Kiingereza) kulia na Madam Secilia (Mwalimu wa Kiswahili).



 HABARI PICHA.










Hitimisho Mwalim mkuu wa shule aliwashukuru waalimu na wazazi kwa ushirikiano na shule kwa ujumla. Pia alimshukuru mgeni rasmi kwa kuja kwa kuthamini mualiko wa kuja kujumuika pamoja na kutambua majukumu mengi aliyo nayo.

KWA MAWASILIANO ZAID ILI KUPATA NAFASI YA MWANANO AMA NDUGU KUJIUNGA NA SHULE YETU



Mkurugenzi wa shule ya secondary Hollywood Mlowo mkoani songwe





    0758-38-08-03




   0756 06 16 99


Mwalimu Mkuu
   
   0755-33-67-55



AHSANTE UNAKARIBISHWA SANA NA MWENYEZI MUNGU AKUBARIKI.

No comments:

Post a Comment