Siku ya tarehe 23 october 2021 itakuwa siku ya kumbukumbu kwa watoto wa shule ya awali / nursery, waalim, wazazi na wanafunzi katika shule ya Hollywood English medium primary school Mlowo Mkoani Songwe.
Hii ni mahafali ya tatu toka shule ilipoanza kutoa elimu ya awali kufanyika ikiwa ni moja ya kitu kinacholeta furaha kwa wanafunzi na kufanya wazazi wengi kutamani watoto wao pia wasome shule ya Hollywood English Medium primary school.
Pichani juu kushoto Mwalim mkuu wa shule ya msingi, katikati muwakilishi wa mgeni rasmi kulia mkurugenzi wa shule za Hollywood Mlowo.
Katika kusheherekea siku hiyo watoto walionesha maonesho mbalimbali kulingana na vipaji vyao, walicheza ngoma za asili, mavazi ya harusi, michezo, maasai. Pia ilisisimua ziadi pale risala iliposomwa kwa ustadi mkubwa na mhitimu wa shule ya awali akipongezwa na wazazi waliofika siku hii.
Mwisho kabisa wahitimu walikula cake ya pamoja na kukabidhiwa zawadi na vyeti vyao vya kuhitim masomo ya awali.
Mungu Ibariki Hollywood,
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ni mwema karibu shule ya Hollywood kwa mafanikio ya mtoto wako.
Mawasiliano Zaidi Mkurugenzi wa shule 0758-97-77-80.